KUKUSANYA SAMPULI YA CHOO KIKUBWA, SAMPULI YA VIMELEA

Sampuli huchanganuliwa kwa vimelea na mayai ya vimelea.

Kukusanya sampuli

Tia choo kikubwa kwenye kontena safi.

Weka sampuli kwenye kontena iliyo na ml 10 za formalin ya 10%.
Ikiwa choo chako kikubwa ni cha majimaji (kutokana na kuendesha), weka kijiko 1 cha sampuli hiyo kwenye kontena na uchanganye vyema. AU
Weka 1/2 kijiko cha sampuli hiyo kwenye kontena na uchanganye vyema. Funga kifuniko cha kontena kwa uthabiti kabisa.

Kuweka maelezo ya utambulisho kwenye sampuli


Tia kontena na neli alama kwa jina

  • lako
  • nambari yako ya ustawi wa jamii (social security)
  • tarehe ya kukusanywa

Kushughulikia na kuhifadhi sampuli


Funganya kontena kwenye mfuko wa plastiki. Unaweza kuhifadhi sampuli hiyo kwenye friji kwa siku tatu. Peleka sampuli kwenye maabara.

Taarifa zaidi


Kwa taarifa zaidi tafadhali wasiliana na kitengo cha huduma kwa wateja cha Fimlab Laboratoriot Oy, simu +358 3 311 74445 katika siku za kazi kuanzia 8.00 hadi 16.00.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

PARASIITIT ULOSTEESTA, SWAHILIN KIELINEN (KUKUSANYA SAMPULI YA CHOO KIKUBWA, SAMPULI YA VIMELEA)